NEWS

Mkenya azua hisia aliposema kwamba angependa kumuoa mjane Collymore

Mkenya mmoja amezua hisia katika mitandao ya kijamii pale aliposema kwamba anaazimia kumuoa mjane wa mwendazake Bob Collymore.

Barobaro huyo ambaye anaonekana kuwa mkaazi wa mashambani maeneo ya Kati anadai kwamba yupo tayari kumrithi Wambui Collymore kama mkewe.

Kijana huyu adai kwamba yuko tayari kumuoa mjane Collymore

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekasirishwa na wengine kuchekeshwa na kijana huyu.

Baadhi ya wafuasi  wamemkashifu wakidai kwamba barobaro huyu anaotea tu mali na fedha ya mjane wa milionea Bob wala hana mapenzi yoyote.

Wengine wamemwita mcheshi na kumwambia hiyo ni ndoto tu aliyonayo isiyoweza kutimizika.

Ni wiki moja tu tangu mwendazake Bob Collymore aage dunia na kumwacha mke na watoto wane. Bob alifariki kwa ugonjwa wa saratani ya damu aliyopigana nayo kwa miaka miwili.

Haya ni baadhi ya maoni yaliyotolewa na wafuasi wake kwenye mtandao wa Facebook.

Maoni ya wafuasi wa kijana huyu aliyetangaza kwamba anampenda mjane Collymore
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
WhatsApp chat