NEWS

Uhuru ashutumu vikali matamshi ya Jaguar kuhusu watanzania – Video

Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta Jumamosi alimkaripia Mbunge wa Starehe Charles Njagua, maarufu kama Jaguar kuhusu matamshi aliyoyaongea ambayo yanakhisiwa kuleta uhasama baina ya wakenya na watanzania.

Kenyatta alinena haya alipozuru Tanzania kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili. Kenyatta alilakiwa na rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Jaguar alitiwa mbaroni tarehe ishini na sita mwezi wa Juni baada ya kutishia watanzania wote wanao fanya biashara katika masoko ya Gikombaa, Kamkunji na kwengineko ya kwamba watashambuliwa na kisha kufurushwa.

“Wengine wanaongea bila kufikiria, mtu amezoea tu kijiji chake hana uzoefu wa kuzuru maeneo mengine, anafikiria kwamba hapo alipo ndipo mwisho wa dunia, ” Uhuru alifoka.

Read Also: Jaguar arrested over xenophobic comments

Matamshi hayo yaliibua kicheko miongoni mwa halaiki iliyokua ikisikiliza hotuba ya marais hao mjini Chato, kaskazini mwa Tanzania.

“Unaskia wengine huko wana ropokwa-ropokwa, unawezaje kumzuia mtanzania asifanye biashara Kenya?” Uhuru aliuliza.

Also Read: Uhuru wants his son to try his luck at a Tanzanian wife

Magufuli ana makao ya kibinafsi huko Chato. Uhuru alisema uhusiano mzuri kati yake na Magufuli utarahisisha mazungumzo mengine kati ya nchi hizi mbili.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
WhatsApp chat