Wednesday, December 1, 2021
spot_imgspot_img
Advertisment
HomeTV47NewDiana Marua afunguka kweli, Churchil akerwa, kunani kati ya Otile na Hamisa...

Diana Marua afunguka kweli, Churchil akerwa, kunani kati ya Otile na Hamisa Mobetto? | TETESI ZA SANAA

Kipi kati ya Otile na Hamisa?

Msanii kutokea nchini Kenya Otile Brown amesafiri wiki hii kuelekea nchini Tanzania kwa kile kinachosemekana kuwa ameelekea +255 kwa ajili ya kufanya collabo  na msanii Juma Jux. Kupitia post ambayo aliweka kwenye page yake ya Instagram, Jux alisema “wakenya mwambieni kijana wenu @otilebrown ajipange #regina video loading…”

Kibao hiki ambacho Otile Brown ameelekea kukiandaa na msanii Jux kipo katika album yake inayofahamika kama “ just in love album”,  album ambayo aliitoa hivi maajuzi– ila kikubwa cha matembezi hayo ni video iliyozagaa mitandaoni ikionyesha Otile akimshika  msanii na fashionista Hamisa Mobetto wengi wakiashiria kolabo kati ya wawili hao. Baadhi ya ngoma  ambazo tayari zimeshatolewa kutoka album hiyo ya Otile Brown ni kama vile “watoto na pombe” aliyomshirikisha Mejja almaarufu “Okwonko “  “dusuma’ aliyomshirikisha Meddy kutoka Rwanda, “hit and run “ aliyomshirikisha khaligraph Jones na “ndaghukunda” aliyomshirikisha Prezzo CMB.

 

Maisha ya Diana kabla ya Bahati

Diana marua, mpenzi wa msanii Kelvin Bahati wiki hii ameweka wazi baadhi ya maswala ambayo wengi hawajui kuhusiana na yeye. Mama huyu wa watoto wawili amesema kuwa alikuwa akiishi maisha ambayo yeye mwenyewe hakufurahishwa nayo ila matatizo ya maisha na kusaka pesa ndiyo yaliyosababisha na ni baadhi ya matukio ambayo hapendi kuyazungumzia. Kupitia chanel yake ya YouTube Diana alisema “I dated guys for money and I had one who paid my rent, another did my house shopping and I had someone to buy me clothes and another to take me out.”

Ila maisha yalibadilika pale alipopatana na Bahati na kwa sasa wana miaka mitano kwenye ndoa na wamebarikiwa na watoto wawili Heaven amabaye ni mtoto wa kike na Majesty wa  kiume

Churchil awaonywa wasanii

Daniel Ndambuki almaarufu kwa jina la ucheshi “Churchil” amewaonywa wacheshi dhidi ya kuweka maisha yao katika mitandao ya kijamii, huku akiwaonya dhidi ya kuwachukua mashabiki wao kama familia. Churchil ambaye alihudhuria mazishi ya mcheshi  Othuol Othuol wikendi iliyopita alisema kuwa nidhamu na kujituma ni vitu vya muhimu katika sanaa. Kupitia video iliyozagaa mitandaoni Churchil alionekana akiwa amekerwa sana na kusema kuwa “ don’t call your fans family because the moment you stop being funny they stop being your family.”

Othuol Othuol aliaga dunia wiki chache zilizopita baada ya kuugua ugonjwa wa “ brain tumour” na alikuwa mmoja wa wacheshi katika kipindi cha Churchil show kinachomilikiwa na mcheshi Churchil

Wachechi wengine waliohudhuria mazishi ya othuol othuol ni kama vile mcheshi jalango, mc jessy terence creative, captain otoyo, jusper murume,sleepy david, teacher wanjiku miongoni mwa wengine.


close


TV47 is on Gotv, DStv, SIGNET, BAMBA and STARTIMES.

Sign up to receive our monthly newsletter.

We don’t spam! Read our privacy policy for more info.

spot_img
RELATED ARTICLES
Advertisment
- Advertisment -

Most Popular

Top Stories

- Advertisement -spot_img

Business