Wednesday, December 8, 2021
spot_imgspot_img
Advertisment
HomeTV47Morning CAFEOpiyo: "Talaka siyo suluhu, ndoa ni kuvumiliana"

Opiyo: “Talaka siyo suluhu, ndoa ni kuvumiliana”

Je, kuna matumaini ya ndoa nzuri siku za usoni? Upendo, maelewano na utamu wa ndoa ulienda wapi? Maswali haya yanatusukuma kutafiti kiini cha matatizo katika ndoa pamoja na kutafuta suluhu ili kuhakikisha ndoa zinadumu na familia bado zinathaminiwa.

Siku ya Jumatatu, Julai 21 katika kipindi cha #MorningCafeTV47, magwiji katika masuala ya ndoa waliwausia wanandoa kwa kuwapatia mawaidha na mwelekeo. Baadhi ya mawaidha walizopeana ni pamoja na kumuelewa mchumba wako kabla ya kuingia kwenye ndoa, kupata wosia na maelekezo kutoka kwa walio na tajriba, na msizitoe siri zenu nje.

“Kila unapoona matatizo katika ndoa, chanzo huwa ni mahusiano ya kimapenzi kabla ya ndoa.” Claytone Tonde alitanguliza kwa kauli hii akisema pasi kuwa na msingi bora unapoanzisha ndoa, haina budi kuvunjika. Misingi inatingika wakati ambapo matumaini na matarajio ya mwanandoa hayajaafikiwa.

Claytone Tonde ni mtaalamu wa masuala ya ndoa.
Changamoto katika ndoa

Kwa upande wake, Elsy Opiyo alidokeza kuwa “kila ua hata kama zuri lina mwiba wake”. Kukosa maelewano, kutokuwa wasikivu, uzinzi, uongo pamoja na masengenyo ya wanandoa ni baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo wanandoa.

Kulingana na Opiyo, talaka siyo suluhisho unapogundua kuwa mchumba wako anazini. Eti uketi kwenye ndoa yako na uweze kujua ni kwa nini mchumba anazini, na mpate suluhu ya kudumu.

Elsy Opiyo, mtaalamu wa ndoa. Anasema talaka haisaidii mpenzi wako akizini.

Tonde aliongeza kuwa chanzo cha changamoto hizi mara nyingi zinatokana na kukosa kuelekezwa na kupata wosia wa kutosha kabla ya kuanza familia, akitaja kwamba asilimia sabini (70%) ya kizazi cha leo wanaishi mjini na hawapati wosia kutoka kwa wazee ikilinganishwa na wale wanopata malezi yao vijijini. “Wanaume ni kama watoto hawataki kusumbuiwa.”

Katika kutamatisha kwao wawili hawa walisisitiza suala la kuwa na ukaribu na uhusiano mwema na wazazi haswa mwanamke ili kuboresha ndoa zao. Opiyo aliwausia wanaume kuwa wasikivu kwa wake zao. Magwiji wote wanashauri kuwa ndoa inahitaji ukomavu, uvumilivu, unyenyekevu, kuelewana na uamuzi dhabiti. Opiyo alitamatisha kwa kusema “hakuna haja ya kusema nipatie talaka, haitakusaidia!”

close

TV47 is on Gotv, DStv, SIGNET, BAMBA and STARTIMES.

Sign up to receive our monthly newsletter.

We don’t spam! Read our privacy policy for more info.

spot_img
RELATED ARTICLES
Advertisment
- Advertisment -

Most Popular

Top Stories

- Advertisement -spot_img

Business